Katika siku ya tano ya maadhimisho ya 'Alfajiri 10 za Ushindi wa
Mapinduzi ya Kiislamu' Jeshi la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran litazindua
kizazi kipya cha vifaru viwili aina ya Zolfaqar na Samsam. Uzinduzi huo
utafanyika katika Jumatatu Februari 4 katika Kituo cha Utafiti na Jihadi
ya Kujitosheleza ya vikosi vya nchi kavu vya Jeshi la Iran.
Aina hii mpya ya vifaru imebuniwa na kutengenezwa kikamilifu na
wataalamu wa Iran. Hii ni katika hali ambayo hapo jana pia Jamhuri ya
Kiislamu ya Iran ilizindua ndege ya kivita yenye umbo pekee duniani
iliyotengenezwa hapa nchini. Ndege hiyo iliyopewa jina la Qaher 313 ina
uwezo wake ni sawa na ndege ya kivita ya Marekani ya F/A 18.
No comments:
Post a Comment