Watu wasiopungua sita wameuawa kufuatia mlipuko wa bomu nje kidogo ya ofisi ya Waziri Mkuu wa Somalia mjini Mogadishu.
Hujuma hiyo imejiri leo Jumanne mchana ambapo kati ya waliouawa ni
maafisa wa usalama. Imearifiwa kuwa mtu aliyekuwa amejifunga mshipi wa
bomu alijiripua karibu na ofiisi ya Waziri Mkuu Abdi Farah Shirdon
katika eneo la kati kati mwa Mogadishu. Maafisa wa usalama wanasema
waziri mkuu alikuwa ofisi wakati wa tukio hilo lakini hakujeruhiwa.
Hakuna kundi lolote lililodai kuhusika na mripuko huo lakini kundi la
kigaidi la al-Shabab limeapa kuipundua serikali ya Somalia.
No comments:
Post a Comment