Mfalme wa Saudi Arabia, amewatishia wakazi wa mji wa Qatifa wa mashariki
mwa nchi hiyo kuwa, atatekeleza mauaji ya umati dhidi yao. Hayo
yameandikwa na mtandao wa habari wa Afkar News ukimnukuu Saud bin Faisal
mmoja wa wanafamilia ya kifalme nchini humo akielezea kuwa, wakazi wa
mji huo wa Qatif wanaishi maisha sawa na wafungwa na kwamba,
watakabiliwa na kifo.
Hii ni katika hali ambayo siku ya Alkhamis
iliyopita Shirika la kutetea Haki za Binaadamu Human Rights Watch
lilitangaza kuwa, mwaka uliopita wa 2012 serikali ya Saudia iliwatia
mbaroni mamia ya wapinzani na wanaharakati wa kisiasa katika maeneo
mbali mbali ya nchi kwa tuhuma za kutangaza misimamo yao ya kisiasa na
kidini inayopingana na kukosoa serikali ya Riyadh. Aidha shirika hilo
lilisisitiza kuwa, wengi wa watu hao waliotiwa mbaroni wamehukumiwa
vifungo bila ya hatia.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment