Waziri wa Ulinzi Misri Jenerali Abdel Fattah al-Sissi ameonya
kuwa mgogoro wa sasa wa kisiasa nchini humo yamkini ukapelekea kuanguka
serikali.
Katika taarifa aliyotoa kupitia ukurasa wake wa Facebook, Jenerali
al-Sissi amesema ‘hali mbaya itaibuka Misri iwapo wanasiasa watashindwa
kutatua hitilafu zao na kukabiliana na mgogoro uliopo.’ Waziri wa Ulinzi
wa Misri halikadhalika ameonya kuwa matatizo ya kiuchumi, kisiasa,
kiusalama na kijamii ni tishio kubwa kwa uthabiti na usalama wa Misri.
Tokea Januari 25 karibu watu 52 wameauwa katika ghasia zilizoibuka
katika miji kadhaa ya Misri ikiwemo mji mkuu Cairo, Alexandria, Suez na
Port Said.
No comments:
Post a Comment