Vikosi vya nchi kavu vya Mali vikisaidiwa na vya Ufaransa vimethibiti
uwanja wa ndege wa Timbuktu na barabara zinazoelekea katika mji huo wa
kihistoria. Luteni Kanali Diarran Kone Waziri wa Ulinzi wa Mali amesema
leo kuwa, uwanja huo wa ndege umedhibitiwa bila makabiliano ya kijeshi.
Taarifa zinasema kuwa waasi wa Mali wamekimbia katika mji huo baada ya
kuchoma moto maktaba zilizokuwa na nyaraka zenye thamani kubwa za kale.
Waziri wa Ulinzi wa Ufaransa amesena kuwa, batalioni za Ufaransa na
vikosi vya Mali vinaelekea katika maeneo ya biashara ya kale na vituo
vya Kiislamu kwenye mji wa Timbuktu ambako inaaminika kuna makaburi ya
watukufu 333 wa Kiislamu ili kuimarisha usalama. Hayo yamejiri baada
ya askari wa Mali na Ufaransa kuukomboa mji wa Gao ulioko mashariki mwa
Timbuktu hapo jana, suala linalohesabiwa kuwa ushindi mkubwa katika
siku 17 za operesheni za kijeshi dhidi ya waasi wa kaskazini mwa Mali.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment