Umoja wa Afrika AU umetangaza kuwa, unafuatilia kwa karibu utekelezwaji
wa mkataba wa amani uliofikiwa hivi karibuni baina ya makundi ya waasi
na serikali ya Jamhuri ya Afrika ya Kati. Ramtane Lamamra, Kamishna wa
Umoja wa Afrika wa Masuala ya Amani na Usalama amesema, umoja huo
unafuatilia kwa karibu utekelezwaji wa mkataba wa amani wa Libreville,
Gabon baina ya makundi ya waasi na serikali ya Rais Francois Bozize wa
Jamhuri ya Afrika ya Kati.
Kwa mujibu wa makubaliano hayo, Rais Bozize
ataendelea kubakia madarakani hadi atakapomaliza muda wake mwaka 2016
lakini hatoruhusiwa kugombea Urais katika uchaguzi ujao. Aidha Rais
Bozize anapaswa kuvunja serikali ya sasa ili kuruhusu kuundwa serikali
ya mpito ambayo itakuwa ni ya umoja wa kitaifa. Kadhalika mkataba huo
unataka Waziri Mkuu achaguliwe kutoka mrengo wa upinzani ambaye
ataongoza serikali ya mpito hadi uchaguzi wa Bunge utakapofanyika katika
kipindi cha miezi kumi na mbili ijayo. Tayari Waziri Mkuu ameshateuliwa
na hivi sasa kinachosubiriwa ni kuundwa serikali ya umoja wa kitaifa
katika nchi hiyo.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment