Rais Jakaya Kikwete wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania amesema kuwa,
kuna njama nyingi za kuzusha machafuko katika nchi hiyo ya Afrika
Mashariki. Rais Kikwete amedai kuwa, kuna watu wanaolipwa ili wachochee
machafuko hayo kwa kutumia mgongo wa dini. Mbali na wanaotumia dini
ambao amesema serikali yake itawadhibiti, Rais Kikwete ameonya kuwa,
hatakubali uchochezi wa vurugu unaofanyika kupitia vyombo vya habari.
Rais Kikwete amesema, hatalifungulia gazeti la Mwanahalisi lililofungiwa
kwa tuhuma za uchochezi. Wakati Rais Kikwete anasema hayo, maeneo ya
mikoa ya Morogoro, Mtwara na Dar es Salaam, hivi karibuni yaligeuka
uwanja wa fujo na vurugu zilizosababisha vifo, majeruhi na uharibifu wa
mali. Aidha juzi hali ya utulivu na amani mkoani Mtwara ilitoweka baada
ya baadhi ya wananchi kuendeleza mapambano na serikali wakipinga gesi
asilia iliyovumbuliwa mkoani humo kusafirishwa kwenda Dar es Salaam bila
kuwanufaisha wao kwanza.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment