Baraza la Amani na Usalama la Umoja wa Afrika limetangaza kuwa, umoja
huo unatarajiwa kutuma vikosi vya kijeshi kaskazini mwa Mali kwa ajili
ya kusaidia operesheni ya kijeshi ya kupambana na makundi ya waasi. Hayo
yamo katika taarifa ya Baraza la Amani na Usalama la Umoja wa Afrika
iliyotolewa jana katika kikao cha wakuu wa AU kinachoendelea mjini Addis
Ababa, Ethiopia. Taarifa hiyo imeeleza kuwa, vikosi hivyo vitatumwa
Mali katika fremu ya kwenda kuungana na vikosi vya Ufaransa na vile vya
Mali katika operesheni ya kijeshi dhidi ya makundi ya waasi ya kaskazini
mwa nchi hiyo. Taarifa hiyo aidha imeitaka serikali ya Mali kuandaa
ramani ya njia na hivyo kuandaa mazingira ya kufanyika uchaguzi huru na
wa kiadilifu katika nchi hiyo ya magharibi mwa Afrika. Baraza la Amani
na Usalama la Umoja wa Afrika limesisitizia udharura wa kuhifadhiwa
umoja wa ardhi ya Mali na kwamba, suala hilo lina umuhimu wa aina yake.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment