Mtu mwingine mmoja ameuawa katika machafuko mapya kati ya
waaandamanaji wa Misri na vikosi vya polisi karibu na maidani ya
at-Tahrir huko Cairo mji mkuu wa nchi hiyo. Rais Muhammad Mursi wa
Misri jana alitangaza hali ya hatari huko Port Said, Suez na Ismailia
baada ya kujiri machafuko makubwa kwenye miji hiyo. Katika juhudi za
kukomesha machafuko huko Misri, serikali ya nchi hiyo imeidhinisha
rasimu ya sheria inayomruhusu Rais kutuma vikosi vya wanajeshi mitaani.
Sheria pia inalipa jeshi la Misri haki ya kuwatia mbaroni raia. Muswada
huo wa sheria unapaswa kwanza kupasishwa na bunge la nchi hiyo.
Akilihutubia taifa kwa njia ya televisheni Rais Mursi amesema hali hiyo
ya hatari itadumu kwa siku 30 kuanzia jana usiku.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment