POLISI leo wamelazimika kupiga mabomu ya machozi kutwa nzima katika kata
ya Chikongola, Manispaa ya Mtwara Mikindani kutawanya wananchi
walioizingira nyumba ya diwani wa kata hiyo Mohamedi Chehako kwa madai
ya kuwahifadhi wachawi ndani ya nyumba yake, huku mwandishi wa habari
mmoja akiripotiwa kujeruhiwa.
Habari ambazo hazijathibitishwa na kamanda wa polisi mkoani hapa, Maria Nzuki zinadai kuwa majira ya saa 10 kasoro za jioni watu wanaodaiwa kuwa ni wanajeshi wa Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ) waliingilia kati na kuanza kutembeza mkong’oto kwa wananchi ili kuzima vuguvugu hilo.
Wananchi walitoa tuhuma hizo baada ya kukuta ungo ikiwa na tunguri ndani yake ambayo inadaiwa kuwa ni ndege ya wachawi uwanjani kwake maeneo ya makaburi Msafa.
Wananchi walijikusanya nyumbani kwa Diwani huyo na kumshinikiza awatoe
wachawi nje ili waweze kuwadhibu, amri iliyopingwa na Diwani huyo.
Kadiri mda ulivyokwenda ndivyo wananchi walivyozidi kuongezeka na
hatimaye kulijitokeza kundi la watu walioanza kutia vurugu, hali
iliyomlazimu Chehako kuomba msaada wa polisi.
Mashuhuda wa tukio walimweleza mwandishi wa habari hizi kuwa polisi
walipofika waliwasihi wananchi kutawanyika kwa kuwa ungo na tunguri zake
zilikuwa zimeteketezwa kwa moto na diwani huyo mbele ya wananchi hao.
1 comment:
Jamani vurugu zitaisha lini tunataka kuwa kama Congo tutulie ili tupate manufaa ya mali ghafi zetu...
Post a Comment