Mahakama katika jimbo la Pennsylvania nchini Marekani imemuhukumu Walter
Meyerle mwenye umri wa miaka 36 adhabu ya kifungo cha miaka 494 jela,
baada ya kupatikana na kosa la kubaka na kuwadhalilisha kijinsia watoto
15 nchini humo. Mahakama hiyo imeeleza kuwa, kuanzia mwaka 1997 hadi
2010 Walter Meyerle aliwabaka watoto wavulana na wasichana wenye umri wa
kati ya miaka 4 na 17. Mwendesha mashtaka wa kesi hiyo amesema kuwa,
idadi kubwa ya watoto hao waliofanyiwa unyama huo walikuwa ni watoto wa
marafiki zake. Wakati huohuo, Mahakama ya Chicago imempiga faini ya dola
laki tano mwalimu Kevin Jones baada ya kupatikana na hatia ya
kuwadhalilisha wanafunzi wake. Mmoja kati ya mwanafunzi aliyekuwa mhanga
wa kutumiwa vibaya kijinsia na mwalimu Kevin Jones alitoa ushadidi wake
huo kwenye mahakama hiyo.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment