Mazungumzo ya kusaka amani kwa ajili ya maeneo ya mashariki mwa
Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo baina ya ujumbe wa waasi wa eneo hilo
na serikali ya Kinshasa yamesimamishwa.
Habari ya kusimamishwa mazungumzo hayo yaliyokuwa yakifanyika Kampala
nchini Uganda imetangazwa na ujumbe wa waasi wa kundi la M23.
Mjumbe wa kundi hilo amesema kuwa mazungumzo hayo yamesimamishwa
baada ya kutokuwepo maendeleo ya aina yoyote. Ameongeza kuwa kikao cha
mwisho baina ya pande hizo mbili kilifanyika tarehe 18 Januari.
Waasi wa Congo wanaituhumu serikali ya nchi hiyo kwamba imepuuza
makubaliano ya amani ya mwaka 2009 na wanadhibiti miji kadhaa muhimu ya
mashariki mwa nchi hiyo. Mwezi Novemba mwaka uliopita kundi hilo la
waasi liliuteka mji wa kistratijia wa Goma kwa siku kadhaa na kulazimika
kuondoka katika mji huo kutokana na mashinikizo ya kieneo na kimataifa.
1 comment:
Kwa nchi ya Congo si rahisi kupata muafaka kwani waliopo madaraka si wazalendo wa nchi yao....
Post a Comment