Manyanyaso dhidi ya Waislamu yanaendelea kushuhudiwa kila leo nchini Ufaransa na bara Ulaya kwa ujumla. Ushahidi wa hivi punde ni kusimamishwa kazi wafanyakazi 4 wa shule moja nchini Ufaransa kutokana na wao kufunga mwezi Mtukufu wa Ramadhani. Meya wa mji wa Gennevilliers ulioko nje kidogo ya mji wa Paris amesema wafanyakazi hao wamesimamishwa kazi baada ya kukiuka vipengee vya mkataba wao.
Meya huyo amesema kwa mujibu wa mkataba, wafanyakazi shuleni humo wanapaswa kula mara tatu wakati wa kazi. Hata hivyo viongozi wa Kiislamu nchini Ufaransa wamelaani hatua hiyo na kutishia kwenda mahakamani kupinga manyanyaso hayo dhidi ya Waislamu. Mashinikizo ya kila kona yamemlazimisha meya huyo kutangaza kuwa atawarudisha kazini wafanyakazi hao Waislamu. Tukio hilo linaonyesha jinsi Waislamu wanavyoendelea kukandamizwa sio tu nchini Ufaransa bali katika bara zima la Ulaya kwa ujumla. Wednesday, August 1, 2012
Wafaransa 4 wafutwa kazi kwa kufunga Ramadhani
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment