Social Icons

twitterfacebookgoogle pluslinkedinrss feedemail

Wednesday, August 1, 2012

Ndege ya kivita ya Marekani yaua watu 35 Somalia

Ndege ya kigaidi isiyo na rubani ya Marekani imetekeleza hujuma mashariki mwa Somalia na kupelekea zaidi ya watu 25 kuuawa. Walioshuhudia wanasema hujuma hiyo imefanyika Jumatano katika wilaya Garas Balley karibu na mji mkuu Mogadishu ambapo watu wengine 40 wamejeruhiwa. Imedaiwa kuwa katika hujuma hiyo vituo viwili vya waasi wa al Shabab vimeharibiwa.
Katika siku za hivi karibuni Marekani imezidisha hujuma zake katika nchi ya Somalia inayokumbwa na njaa, Kwa muda mrefu sasa Marekani imekuwa ikitumia ndege zisizo na rubani kushambulia raia huko Pakistan, Afghanistan, Yemen na Somalia kwa madai ya kukabiliana na magaidi. Hata hivyo raia wa kawaida ndio wahanga wakuu wa mashambulio hayo ya Marekani. Umoja wa Mataifa umelaani hujuma ya ndege hizo za kigaidi za Marekani na kusema ni ukiukwaji wa sheria za kimataifa.

No comments: