Waziri wa Ulinzi wa Marekani, Leon Panetta amesema ziara yake katika utawala haramu wa Israel haina lengo la kujadili masuala ya Iran. Panetta ambaye hapo jana alikuwa Misri alilipongeza Baraza la Kijeshi kwa kukubali kukabidhi madaraka kwa utawala wa kiraia. Waziri wa Ulinzi wa Marekani ameelekea Tel Aviv na tayari amekutana na Waziri wa Vita wa utawala huo ghasibu, Ehud Barack.
Panetta amekanusha madai ya vyombo vya habari kwamba kadhia ya nyuklia ya Iran ilikua miongoni mwa ajenda muhimu kwenye mazungumzo yake na Ehud Barack. Wamagharibi pamoja na Wazayuni wamekuwa wakieneza uongo na propaganda kwamba Iran iko mbioni kuunda bomu la nyuklia. Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imekuwa ikisisitiza kuwa miradi yake ya nyuklia ni ya amani na inafanyika chini ya uangalizi wa Wakala wa Kimataifa wa Nishati ya Atomiki IAEA. Wednesday, August 1, 2012
Panetta: Sitojadili masuala ya Iran huko Israel
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment