Vikosi vya usalama vya Somalia vimewapiga risasi na kuwaua watu wawili waliokusudia kuripua jengo linalofanyika kikao cha waasisi wa Somalia kwa ajili ya kupasisha rasimu ya katiba mpya ya nchi hiyo. Yassin Abdi, mmoja wa maafisa wa ngazi za juu wa polisi ya Somalia amesema kuwa, vikosi vya usalama vya nchi hiyo vimefanikiwa kuwaua watu hao waliokuwa na nia ya kujiripua kwa mabomu ndani ya ukombi kunakoendelea kikao cha waasisi wa Somalia kwa ajili ya kupasisha rasimu ya katiba mpya ya nchi hiyo.
Amesema, baada ya watu hao kufyatuliwa risasi na polisi ndipo mabomu waliyokuwa wameyavaa yaliporipuka. Ameongeza kuwa, mbali na watu wawili hao kuuawa, polisi mmoja pia ameuawa katika tukio hilo. Tayari wajumbe wanaohudhuria kikao hicho wapatao 825 wamepitisha rasimu ya katiba mpya ya Somalia hatua ambayo inahesabiwa kuwa muhimu zaidi katika kumaliza vita vya ndani nchini humo. Wednesday, August 1, 2012
Kufeli njama ya kulipua kikao cha katiba Somalia
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment