Rais Bashar al-Assad wa Syria amesema nchi yake iko katika vita ‘vikali na vya kishujaa’ ambavyo vitaainisha hatima ya taifa. Akizungumza kwa mnasaba wa mwaka wa 67 wa kuanzishwa jeshi la Syria, Assad amesema maadui wameingia miongoni mwa wananchi kwa lengo la kuvuruga usalama lakini wameshangazwa kuona namna wananchi hao walivyosimama kidete na kuvunja njama zao.
Assad amelipongeza jeshi la Syria kwa kusimama kidete katika kukabiliana na magenge ya kigaidi nchini humo. Amelitaja jeshi hilo kuwa ni ‘uti wa mgongo’ wa taifa la Syria. Hotuba ya Assad inakuja wakati ambao vikosi vya Syria vinapambana vikali na magenge ya magaidi wanaoungwa mkono na nchi za kigeni katika maeneo mbali mbali ya nchi hiyo. Jeshi la Syria limefanikiwa kuwatimua magaidi kutoka aghlabu ya maeneo ya mji wa Aleppo. Katika upande mwingine Serikali ya Syria imetuma barua mbili tofauti kwa Mwenyekiti wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa na kwa Katibu Mkuu wa Umoja huo Ban Ki moon, zikifichua zaidi njama mbalimbali zinazofanywa dhidi ya nchi hiyo. Katika barua hizo, serikali ya Syria imezituhumu moja kwa moja nchi za Saudi Arabia, Qatar, Uturuki na baadhi ya madola ya Magharibi kuwa zinawaunga mkono magaidi wanaotenda jinai nchini humo. Wednesday, August 1, 2012
Assad: Syria iko katika vita muhimu
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment