Kaimu rais wa Ghana, John Dramani Mahama amemteua Gavana wa Benki Kuu ya nchi hiyo kuwa makamu wa rais. Taarifa kutoka ofisi ya Mahana imesema kwamba, Kwesi Amissah-Arthur ameteuliwa na jina lake litawasilishwa mbele ya kamati ya bunge inayohusika na kuidhinisha maafisa wa serikali walioteuliwa ili kuidhinishwa rasmi.
Duru za karibu na ofisi ya rais zinasema kuwa huenda Mahana pia akamchagua Kwesi kuwa mgombea mwenza kwenye uchaguzi mkuu ujao baadaye mwezi Disemba mwaka huu. Dramani Mahana alichukua hatamu za uongozi kufuatia kufariki dunia hayati John Atta Mills siku chache zilizopita. Kifo cha Rais Mills kimebadilisha kabisa muundo wa kisiasa kwani kiongozi huyo alitarajiwa kugombea urais kwa kipindi kingine cha pili kwenye uchaguzi mkuu ujao. Wednesday, August 1, 2012
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment