Kitengo cha kimataifa katika maonyesho ya kimataifa ya Qur'ani Takatifu ya mjini Tehran kimefunguliwa. Sherehe za ufunguzi wa kitengo hicho zimehudhuriwa na wasanii wa masuala ya Qur'ani kutoka nchi 10 duniani, wahakiki wa sayansi ya Qur'ani wa Irani na viongozi wa ngazi za juu wa masuala ya Qur'ani na utamaduni hapa nchini. Kitengo hicho kinaonyesha kazi zaidi ya wasanii 80 wa kaligrafia na sanaa ya uchoraji unaohusiana na masuala yaliyozungumziwa katika Qur'ani na wahakiki mashuhri wa taaluma ya Qur'ani.
Wasanii na wanakaligrafia kutoka nchi mbalimbali zikiwemo Bangladesh, Afghanistan, Russia, Ufilipino, Pakistan, Ghana, Algeria, Uturuki, Lebanon, Bosnia na Syria wanaonyesha kazi zao katika kitengo hicho. Kitengo hicho cha kimataifa kitaendelea kuwa wazi kwa muda wa siku 10 ambapo watafiti, waandishi na wachapishaji wa Qur'ani Tukufu na vitabu vingine vinavyohusiana na sayansi ya kitabu hicho kitakatifu kutoka nchi za kigeni watawasilisha kazi zao. Wasomi, wasanii na shakhsia wa Qur'ani kutoka nchi tofauti za dunia wamealikwa kushiriki katika shughuli za kitengo hicho. Tuesday, July 31, 2012
Kitengo cha kimataifa maonyesho ya Qur'ani Tehran chafunguliwa
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment