Social Icons

twitterfacebookgoogle pluslinkedinrss feedemail

Tuesday, July 31, 2012

Uturuki yasisitizia uwezekano wa kuingilia kijeshi Syria

Waziri wa Mambo ya Nje wa Uturuki ameripoti juu ya uwezekano wa kuingilia kijeshi nchi hiyo huko Syria. Ahmad Dawood Oglu amedai kuwa wanajeshi na idara za ujasusi za Uturuki wameshayatambua maeneo yote ya Syria  na kwamba Uturuki itatoa jibu kali kwa kitisho chochote iwapo maslahi yake yatatishiwa huko Syria.
Waziri wa Mambo ya Nje wa Uturuki ameashiria pia kuongezeka wimbi la wakimbizi wa Syria huko Uturuki na kueleza kuwa jeshi la Uturuki litaingia huko Syria na kuanzisha eneo alilodai kuwa ni la amani kati ya mpaka wa nchi hiyo na Uturuki, iwapo idadi ya wakimbizi hao itapindukia laki moja. Waziri wa Mambo ya Nje wa Uturuki ametoa madai hayo katika hali ambayo katika siku na wiki kadhaa zilizopita jeshi la nchi hiyo pia lilituma vifaru vingi na silaha nzito nyingine kwenye maeneo ya mpaka wa nchi hiyo na Syria na hivyo kuzidisha operesheni zake za kijasusi kwa kutumia ndege zake za ujasusi katika maeneo mbalimbali ya kwenye mpaka wa Uturuki na Syria.

No comments: