Social Icons

twitterfacebookgoogle pluslinkedinrss feedemail

Tuesday, July 31, 2012

Ebola yaua 14 nchini Uganda


Maafisa wa afya nchini Uganda wametangaza kuwa ugonjwa wa ebola umesababisha vifo vya watu 14 nchini humo. Watu hao wamefariki dunia katika kipindi cha mwezi mmoja uliopita kwenye maeneo ya magharibi mwa Uganda.
Shirika la Afya Duniani (WHO) na maafisa wa serikali ya Uganda wamethibitisha kwamba ugonjwa wa ebola unaenea kwa kasi nchini humo. Wataalamu wa magonjwa ya kuambukiza wanatahadharisha kwamba ugonjwa huo hatari huenda ukasambaa na kuingia katika nchi jirani. Zaidi ya watu 224 walifariki dunia nchini Uganda kutokana na ugonjwa wa ebola hapo mwaka 2000. Ugonjwa huo ambao unasababishwa na kirusi uligunduliwa kwa mara ya kwanza mwaka 1976 katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo na bado haujapatiwa kinga.

No comments: