Rais Omar al Bashir wa Sudan amekataa mwaliko uliotolewa na Umoja wa Afrika kwa ajili ya kukutana na Rais Silva Kiir wa Sudan Kusini hapo kesho kwa lengo la kupeleka mbele mazungumo ya kumaliza hitilafu za pande mbili. El Obeid Morawah msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Sudan amesema, al Bashir amekataa mwaliko huo kwa sababu tayari alikuwa amepanga kuitembelea Qatar na kwamba Khartoum inaona bora mkutano kama huo ufanyike baada ya kuandaliwa vyema.
Pande hizo mbili zimefikia makubaliano ya awali kuhusiana na suala la usafirishaji mafuta ya Sudan Kusini kupitia mabomba ya Sudan lakini bado makubaliano ya mwisho hayajafikiwa. Mazungumzo hayo yanasimamaiwa na Umoja wa Afrika chini ya upatanishi wa Thabo Mbeki rais wa zamani wa Afrika Kusini. Tuesday, July 31, 2012
Al Bashir akataa kukutana na Rais wa Sudan Kusini
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment