Social Icons

twitterfacebookgoogle pluslinkedinrss feedemail

Tuesday, July 31, 2012

Iran: Kuimarishwa amani kuna faida kwa nchi zote

Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran amesema, serikali na wananchi wa Iran wamekuwa marafiki na jirani mwema kwa serikali na taifa la Iraq na kwamba kuimarishwa amani na usalama katika njanya zote kwenye eneo hili ni kwa maslahi ya nchi zote.
Ali Akbar Salehi amesema hayo leo alipokutana na kuzungumza na Liwaa Sumaisem Waziri wa Utalii na Turathi wa Iraq. Sambamba na kusisitiza hamu na shauku ya wananchi wa Iran ya kupenda kuitembelea Iraq na hasa kuzuru maeneo matukufu na makaburi ya Maimamu Watoharifu nchini humo, Salehi ameelezea kuwa ana matumaini kuwa kwa kutekelezwa makubaliano ya pande mbili na kuondolewa baadhi ya vikwazo na matatizo kutashuhudiwa kupanuka na kurahisishwa mahusiano na maingiliano ya kidugu kati ya Wairaq na Wairani. Kwa upande wake Waziri wa Utalii na Turathi wa Iraq ameashiria mazungumzo na mijadala mizuri aliyofanya na maafisa wa Iran na kuelezea matumaini yake kuwa, kutokana na makubaliano yaliyofikiwa safari za wananchi wa pande mbili za kutembelea nchi hizo zitarahisishwa na kuongezeka haraka iwezekanavyo.

No comments: