Mkuu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhdumia wakimbizi UNHCR Antonio Guterres amesema migogoro mipya iliongezeka mwaka jana na kusababisha wimbi kubwa la wakimbizi wapya katika muongo uliopita.
Akizungumza katika uzinduzi wa ripoti ya hali ya wakimbizi duniani Alhamisi, Antonio Guterres amesema ripoti hiyo sio kitabu kuhusu takwimu bali ni uchambuzi wa tatizo la wakimbizi na changamoto za kuwasaidia wakimbizi hao. Guterres ametaja migogoro mitatu aliyosema ni mibaya sana ambayo ni ya Syria, Sudan Kusini na Sudan pamoja na Mali. Ameongeza kuwa watu pia wamekuwa wakikimbia Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo kuingia Uganda na Rwanda.
Mkuu huyo wa UNHCR ameongeza kuwa huku migogoro mipya ikizuka ya zamani haitoweki. Ameashiria migogoro ya zamani inayoendelea huko Afghanistan, Somalia na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo. Aidha amegusia idadi kubwa ya Wapalestina ambao ardhi zao zinakaliwa kwa mabavu na utawala haramu wa Israel.

No comments:
Post a Comment