Social Icons

twitterfacebookgoogle pluslinkedinrss feedemail

Thursday, May 31, 2012

AU: Tutapeleka suala la Mali katika Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa

Umoja wa Afrika AU umetangaza kuwa, utapeleka suala la mgogoro wa Mali katika Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa ili zichukuliwe hatua mwafaka. Hayo yamesemwa na afisa mmoja wa karibu na mwenyekiti wa umoja huo na kuongeza kuwa AU imeazimia kulifikisha suala hilo katika Baraza la Usalama, katika hatua ya kutaka kumaliza mgogoro unaoendelea nchini Mali. Afisa huyo ambaye hakutaka jina lake litajwe amesema kuwa, Umoja wa Afrika utaliomba baraza hilo kutoa azimio ambalo litailetea manufaa nchi hiyo. Hata hivyo afisa huyo amesema, bado haijaainishwa ni lini suala hilo litawasilishwa katika baraza hilo. Nchi ya Mali ambayo ilikuwa ikipigiwa mfano bora wa demokrasia barani Afrika, mapema mwezi Machi ilishuhudia mapinduzi ya kijeshi, hali iliyopelekea nchi hiyo kuzongwa na migogoro ya ndani hadi sasa.

No comments: