Muhammad Reza Rahimi, Makamu wa kwanza wa Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amekamilisha safari yake ya kuzitembelea nchi za Kenya na Tanzania kwa kusaini hati kumi za ushirikiano kati ya Iran na nchi hizo za Afrika Mashariki.
Katika sehemu ya kwanza ya safari yake hiyo, siku ya Jumatatu, Makamu wa kwanza wa Rais wa Iran aliwasili mji mkuu wa Kenya Nairobi na siku ya Jumatano akaelekea Dar es Salaam mji mkuu wa kibiashara wa Tanzania ambapo katika safari yake ya siku moja nchini humo alikutana na kufanya mazungumzo na Rais Jakaya Kikwete pamoja na mwenyeji wake Makamu wa Rais wa Tanzania Dakta Mohammed Gharib Bilal ambapo pande mbili za Tehran na Dar es Salaam zilibadilishana mawazo juu ya namna ya kustawisha zaidi ushirikiano kwa manufaa ya kiuchumi ya nchi mbili. Katika mazungumzo yake na Kikwete, Rahimi sambamba na kuelezea nia ya dhati ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ya kustawisha uhusiano wake na Tanzania kufikia kiwango cha juu kabisa kupitia utiaji saini mikataba na hati za ushirikiano katika nyanja mbalimbali, alisisitiza kwamba ushirikiano huo baina ya nchi mbili unaweza kuwa na taathira nzuri katika kustawisha uchumi wa Tanzania. Kwa upande wake, Rais wa Tanzania aliipongeza Iran kwa maendeleo iliyopata katika nyanja mbalimbali na jinsi ilivyofanikiwa kukabiliana na vikwazo vya maadui na kueleza kwamba Tanzania iko tayari kufaidika na tajiriba ya mafanikio ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran. Katika mazungumzo yake na Makamu wa Rais wa Tanzania, Rahimi aliashiria jinsi Iran inavyoguswa na kuyapa umuhimu maslahi ya mataifa ya Afrika na kubainisha kuwa mataifa ya bara la Afrika yana nafasi maalumu mbele ya serikali na wananchi wa Iran.
Baada ya mazungumzo kati ya Makamu wa kwanza wa Rais wa Iran na viongozi wa Tanzania pande hizo mbili zilisaini hati sita za maelewano na ushirikiano katika sekta kadhaa ukiwemo wa baina ya vyama vya wafanya biashara wa nchi mbili, ushirikiano wa maendeleo na ushajiishaji na utoaji msukumo katika uwekezaji. Katika sehemu ya kwanza ya safari yake hiyo, siku ya Jumatatu, Makamu wa kwanza wa Rais wa Iran aliwasili mji mkuu wa Kenya Nairobi na siku ya Jumatano akaelekea Dar es Salaam mji mkuu wa kibiashara wa Tanzania ambapo katika safari yake ya siku moja nchini humo alikutana na kufanya mazungumzo na Rais Jakaya Kikwete pamoja na mwenyeji wake Makamu wa Rais wa Tanzania Dakta Mohammed Gharib Bilal ambapo pande mbili za Tehran na Dar es Salaam zilibadilishana mawazo juu ya namna ya kustawisha zaidi ushirikiano kwa manufaa ya kiuchumi ya nchi mbili. Katika mazungumzo yake na Kikwete, Rahimi sambamba na kuelezea nia ya dhati ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ya kustawisha uhusiano wake na Tanzania kufikia kiwango cha juu kabisa kupitia utiaji saini mikataba na hati za ushirikiano katika nyanja mbalimbali, alisisitiza kwamba ushirikiano huo baina ya nchi mbili unaweza kuwa na taathira nzuri katika kustawisha uchumi wa Tanzania. Kwa upande wake, Rais wa Tanzania aliipongeza Iran kwa maendeleo iliyopata katika nyanja mbalimbali na jinsi ilivyofanikiwa kukabiliana na vikwazo vya maadui na kueleza kwamba Tanzania iko tayari kufaidika na tajiriba ya mafanikio ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran. Katika mazungumzo yake na Makamu wa Rais wa Tanzania, Rahimi aliashiria jinsi Iran inavyoguswa na kuyapa umuhimu maslahi ya mataifa ya Afrika na kubainisha kuwa mataifa ya bara la Afrika yana nafasi maalumu mbele ya serikali na wananchi wa Iran.
Kabla ya safari yake ya Tanzania, siku ya Jumatatu iliyopita Makamu wa kwanza wa Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran aliwasili mjini Nairobi ambapo katika mazungumzo yake na Waziri Mkuu wa Kenya Raila Odinga alikaribisha hatua za kustawisha ushirikiano baina ya nchi mbili katika nyuga mbalimbali na hasa ya uchumi. Naye Waziri Mkuu wa Kenya alikaribisha makubaliano yaliyosainiwa kati ya Tehran na Nairobi kwa lengo la kuleta uwiyano wa mizani ya kibiashara baina ya pande mbili. Hati nne za maelewano zilisainiwa kwa lengo la kuimarisha zaidi ushirikiano wa kiuchumi kati ya Iran na Kenya na kustawisha kiwango cha uhusiano baina ya pande mbili. Hati hizo zinajumuisha mashirikiano katika masuala ya ushuru, umeme, usambazaji maji na kuondoa utozaji kodi za ziada. Katika miaka ya hivi karibuni Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imekuwa na mtazamo maalumu juu ya suala la kustawisha ushirikiano na nchi za Kiafrika ambapo hadi sasa hatua kadhaa zimechukuliwa na jitihada nyingi zimefanyika katika uwanja huo.../
No comments:
Post a Comment