Muhammad Mursi, mgombea urais wa Misri kwa tiketi ya chama cha Uhuru na Uadilifu, tawi la kisiasa la harakati ya Ikhwanul Muslimin ametoa wito kwa wagombea walioshindwa katika duru ya kwanza ya uchaguzi huo kumuunga mkono katika duru ya pili ya kinyang'anyiro hicho. Mursi amesema uungaji mkono wa Abdel Moneim Aboul Fotouh, Hamdeen Sabahi, Mohammed Salim Al-Awa, Abdullah al-Ashaal, and Khaled Ali unahitajika kwa ajili ya kuelekea kwenye uthabiti, uhuru wa kweli, Misri mpya na kufikiwa malengo ya taifa na mapinduzi. Katika duru ya pili ya uchaguzi wa rais itakayofanyika tarehe 16 na 17 mwezi huu, Muhammad Mursi atachuana na Ahmad Shafiq, Waziri Mkuu wa mwisho wa utawala uliong'olewa kwa mapinduzi ya wananchi wa dikteta Hosni Mubarak. Hii ni katika hali ambayo sheria iliyopasishwa mwezi Aprili na bunge la Misri inapiga marufuku viongozi wote waliohudumu katika utawala wa Mubarak kushikilia nyadhifa za kisiasa. Mahakama ya Katiba ambayo inaichunguza sheria hiyo itatoa uamuzi wake tarehe 12 ya mwezi huu wa Juni. Endapo ugombeaji wa Ahmad Shafiq utabatilishwa, Muhammad Mursi atachuana na Hamdeen Sabahi katika duru hiyo ya pili.../
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment