Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limekaribisha hatua ya Sudan na Sudan Kusini kuondoa vikosi vya majeshi yao katika eneo zinalozozania la Abyei na kuzishajiisha kutekeleza wajibu wao kuhusiana na azimio la baraza hilo. Taarifa iliyotolewa na Baraza la Usalama imeeleza kuwa nchi wanachama za baraza hilo zimekaribisha hatua ya kuondolewa vikosi vya Sudan na Sudan Kusini katika eneo la mpakani la Abyei lakini zinasisitiza kwamba uondoaji huo unapasa kujumuisha pia vikosi vya Polisi. Baada ya kujitokeza uwezekano wa kuzuka vita kamili kati ya nchi jirani za Sudan na Sudan Kusini, Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa lilizitaka nchi hizo mbili kuweka kando hitilafu zao na kufanya mazungumzo juu ya masuala muhimu zinayozozania ikiwemo hatima ya eneo lenye utajiri wa mafuta la Abyei.../
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment