skip to main |
skip to sidebar
Mkutano wa kujadili mustakabali wa Afghanistan waanza mjini Kabul
Mkutano mkubwa wa kujadili mustakabali wa Afghanistan umeanza mjini Kabul leo Alkhamisi. Jamhuri ya Kiislamu ya Iran inawakilishwa na Waziri wake wa Mambo ya Nje, Ali Akbar Salehi ambaye amesema punde baada ya kuwasili mjini Kabul kwamba, Tehran inaunga mkono pamoja na kukaribisha juhudi zozote za kimataifa zenye lengo la kuimarisha usalama nchini Afghanistan hususan hatua ya kuyaondoa majeshi ya kigeni nchini humo. Salehi amesema matatizo ya Afghanistan yamekuwa mazito zaidi kutokana na uwepo wa majeshi ya kigeni katika nchi hiyo. Rais Hamid Karzai wa Afghanistan amesema kwenye hotuba yake ya ufunguzi kwamba, nchi za eneo zina uwezo wa hali na mali wa kutatua matatizo yao bila kuingiliwa na wageni. Karzai amesema Waafghani wana hamu ya kuona majeshi vamizi yakiondoka katika ardhi yao. Kiongozi huyo pia amekaribisha hatua ya Ufaransa ya kuahidi kuondoa majeshi yake nchini Afghanistan kufikia mwishoni mwa mwaka huu.
No comments:
Post a Comment