Social Icons

twitterfacebookgoogle pluslinkedinrss feedemail

Friday, June 1, 2012

Gazeti la Kizayuni lakiri kuwa jeshi la Israel ni dhaifu kuweza kukabiliana na Iran

Gazeti la Kizayuni la Yediot Ahronot limeashiria udhaifu wa jeshi la utawala wa Kizayuni wa Israel na kukiri kuwa jeshi hilo halina uwezo wa kukabiliana na Iran. Sambamba na kusisitiza kuwa vitisho vya kufanya mashambulio ya kijeshi dhidi ya Iran vinavyotolewa na baadhi ya viongozi wa Kizayuni ni vya kipropaganda na vya utiaji chumvi, Yediot Ahronot limeandika kuwa Israel haina vikosi na silaha zinazohitajika kuweza kukabiliana na Iran. Gazeti hilo limeongeza kuwa endapo Israel itaanzisha uchokozi dhidi ya Iran itakabiliwa na radiamali kali ya Tehran na pia ya makundi ya muqawama katika eneo la Mashariki ya Kati ikiwemo Hizbullah. Wakati huohuo mkuu wa zamani wa shirika la ujasusi la Israel Mossad Meir Dagan amekiri kuwa Israel haina uwezo mkubwa wa kukabiliana na Iran. Sambamba na kusisitiza tena msimamo wake wa kupinga uchukuaji wa hatua yoyote ya kijeshi dhidi ya Iran Dagan amesema hatua hiyo itawafanya wananchi wa Iran wauunge mkono zaidi Mfumo wa Jamhuri ya Kiislamu.../

No comments: