![]() |
Waziri wa Mambo ya nje wa Uingereza |
Katika kukaribia duru nyingine ya mazungumzo kati ya Iran na kundi la 5+1, Waziri wa Mambo ya Nje wa Uingereza ametishia kwamba Tehran itawekewa vikwazo zaidi iwapo eti haitachukua 'hatua halisi ' kuhusiana na mipango yake ya nyuklia. William Hague amesema kwamba, wanasubiri hatua halisi na mapendekezo kutoka kwa Iran kuhusu suala hilo, na kwamba kama hayo hayatokuwepo vikwazo vitazidishwa dhidi ya Tehran. Tangu mwanzoni mwa mwaka huu wa 2012 Marekani na Umoja wa nchi za Ulaya zimeiwekea Iran vikwazo vya fedha na katika sekta ya mafuta, zikidai kuwa mipango ya nyuklia ya Iran ni kwa ajili ya malengo ya kijeshi. Iran inasema kuwa, kwa kuwa imesaini Mkataba wa Kuzuia Uzalishaji na Uenezaji wa Silaha za Nyuklia NPT na ni mwanachama wa Wakala wa Kimataifa wa Nishati ya Atomiki IAEA, ina haki ya kustafidi na teknolojia ya nyuklia kwa malengo ya amani.
No comments:
Post a Comment