Watu tisa wameuawa kufuatia hujuma nne za mabomu katika maeneo tafauti ya mji mkuu wa Somalia, Mogadishu.
Katika hujuma hizo za Jumamosi, wanajeshi sita wa serikali ya mpito wameuawa wakati wakilinda doria katika kijiji cha Gubta-gar.
Mlipuko mwingine umejiri katika kijiji cha Gubadley na kupelekea wanajeshi wawili wa Kikosi cha Kulinda Amani cha Umoja wa Afrika AMISOM kuuawa.
Kwingineko katika mashambulio mawili ya guruneti, watu watatu wameuawa na wengine kadhaa kujeruhiwa katika soko la Bakara karibu na Msikiti wa Abdalla Shideye. Hakuna kundi lolote lililodai kuhusika na hujuma hizo lakini wakuu wa Serikali ya Mpito ya Somalia TFG wanawalaumu waasi wa kundi la al-Shabab kuwa ndio waliohusika.

No comments:
Post a Comment