Social Icons

twitterfacebookgoogle pluslinkedinrss feedemail

Sunday, May 20, 2012

Njama ya kutenganisha Darfur na Sudan zabainika

Mshauri wa Rais wa Sudan amesema Marekani inapanga njama ya kutenganisha eneo la Darfur na Sudan.
Nafi Ali Nafi amenukuliwa na televisheni ya Al Alam akisema kuwa Roger Winter Mmarekani aliyewasaidia waasi wa Sudan Kusini katika vita vyao vya kujitenga na Sudan sasa amepewa jukumu la kusimamia kundi la waasi wa Darfur lijulikanalo kama SLA.
Kwa mujibu wa Ali Nafi, Roger Winter amenukuliwa akisema kuwa, ‘kazi ya kusini imemalizika na sasa ni wakati wa Darfur.'
Weledi wa mambo wanasema kuwa uchochezi wa Marekani na Utawala wa Kizayuni wa Israel ndio uliopelekea Sudan Kusini kujitenga na Sudan.
Utawala wa Sudan Kusini unaendeleza uchokozi dhidi ya Sudan na katika tukio la hivi karibuni vikosi vya Juba viliuhujumu na kuukalia kwa mabavu mji wenye utajiri wa mafuta wa Heglig kabla ya kutimuliwa na vikosi vya Khartoum.

No comments: