Social Icons

twitterfacebookgoogle pluslinkedinrss feedemail

Saturday, May 26, 2012

Wanajeshi wa Uingereza waliruhusiwa kumuua mtu mweusi yeyote nchini Kenya

Katika habari iliyochapishwa na gazeti la The Guardian la nchini Uingereza kuhusiana na siasa za Uingereza katika kipindi cha ukame wa India kilichopelekea kuwa wahanga watu wapatao milioni 29 nchini humo gazeti hilo la Guardian limeandika kuwa, wanajeshi wa Uingereza nchini Kenya walipewa idhini ya kumuua mtu yeyote mweusi wakitaka. Gazeti hilo limeendelea kuandika kuwa, katika kipindi cha harakati za mapinduzi ya Mau mau za mwaka 1950 nchini Kenya wanajeshi wa Uingereza waliwafukuza wananchi wa kabila la Kikuyu kutoka katika ardhi zao sambamba na kuwapiga marufuku kikamilifu kujishughulisha kwa namna yoyote na siasa ambazo zingepelekea kupata uhuru wao. Utawala wa Kiingereza wa wakati huo uliamua kwa makusudi kuwahamisha na kuwapeleka katika makambi maalumu kwa nguvu watu wapatao laki tatu na ishirini elfu nchini humo. Mbali na hayo watu wengine wapatao milioni moja waliwekewa vikwazo sambamba na kuwakata masikio wafungwa huku wengine wakiuawa kwa kumiminiwa risasi bila hatia. Ripoti hiyo inaonyesha kuwa Wakikuyu wapatao laki moja waliuawa na Waingereza ima kwa risasi au kwa njaa sambamba na kuwanyonga wengine wapatao 1090.

No comments: