Social Icons

twitterfacebookgoogle pluslinkedinrss feedemail

Tuesday, May 29, 2012

Wamarekani weusi wabanwa na sheria mpya za uchaguzi


Rep. Emanuel Cleaver (D-MO)
Rep. Emanuel Cleaver Mjumbe wa Baraza la Congress (CBC).
Wajumbe Weusi katika Baraza la Congress (CBC) nchini Marekani wameitisha mkutano wa kitaifa kujadili sheria mpya za kadi za kupigia kura ambazo zinaonekana kuwadhoofisha wapiga kura weusi au wenye asili ya Afrika nchini humo.
Press TV imeripoti kuwa, huenda idadi kubwa ya Wamarekani weusi wakashindwa kupiga kura katika uchaguzi wa rais mwezi Novemba kutokana na sheria ambazo zimepitishwa katika majimbo kadhaa. Kwa mujibu wa sheria hiyo, kila mpiga kura anapaswa kuwa na kadi maalumu ya upigaji kura katika hali ambayo huko nyuma kura zimekuwa zikipigwa bila kadi hiyo.
Taasisi ya Utafiti ya Brennan Center imesema sheria ya kadi ya kura itawaathiri vibaya Wamarekani weusi. Aidha baadhi ya majimbo ya Marekani yamepitisha sheria za kubana harakati za kushajiisha uandikishaji wapiga kura zilizokuwa zikitekelezwa na makundi ya wanawake na Wamarekani weusi.

No comments: