Social Icons

twitterfacebookgoogle pluslinkedinrss feedemail

Saturday, May 26, 2012

Sudan yawasilisha mashtaka UN dhidi ya Sudan Kusini

Balozi na mwakilishi wa kudumu wa Sudan katika Umoja wa Mataifa, amewasilisha mashtaka ya nchi yake dhidi ya hatua za kichokozi za Sudan Kusini. Dafullah Al Haj Ali amewasilisha mashtaka hayo leo na kuongeza kuwa, katika kipindi cha siku nane zilizopita kwa mara kadhaa vikosi vya Sudan Kusini vimefanya uvamizi katika maeneo ya mpakani ya Sudan na kukiuka azimio nambari 2046 la Umoja wa Mataifa.
Aidha mashtaka hayo yameitaka serikali ya Juba kuheshimu kikamilifu mamlaka ya ardhi ya Sudan. Mashtaka hayo yamewasilishwa katika hali ambayo Umoja wa Mataifa umearifiwa kuwa serikali za Juba na Khartoum zinatarajia kukutana siku ya Jumanne mjini Addis Ababa Ethiopia kwa mazungumzo ya kutatua mgogoro uliopo kati ya nchi mbili hizo. Mgogoro kati ya Sudan na Sudan Kusini ulianza baada ya vikosi vya serikali ya Juba kuvamia eneo la Heglig ambalo ni mali ya Sudan.

No comments: