skip to main |
skip to sidebar
UN yaisaidia Senegal kukabiliana na baa la njaa linaloikabili
Naibu wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa ametangaza kuwa, Umoja huo umeisaidia serikali ya Senegal kiasi cha dola milioni saba kwa ajili ya kukabiliana na njaa nchini humo. Valerie Amos Naibu wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa anayeshughulikia masuala ya huduma za kibinadamu ya Umoja huo amesema, fedha hizo zitagawanywa katika taasisi tofauti za Umoja huo mjini Dakar Senegal ili kuisaidia serikali ya nchi hiyo majukumu makubwa iliyonayo. Amos ameyasema hayo katika kikao cha pamoja na Abdoul Mbaye Waziri Mkuu wa Senegal kilichofanyika katika mji mkuu wa nchi hiyo. Naibu huyo wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa atakutana pia na Rais wa nchi hiyo Macky Sall na kujadili njia za kulitafutia ufumbuzi suala la uhaba wa chakula linaloikabili nchi hiyo hivi sasa.
No comments:
Post a Comment