Social Icons

twitterfacebookgoogle pluslinkedinrss feedemail

Saturday, May 26, 2012

Hizbullah: Wapinzani wanataka kuing'oa serikali ya Lebanon

Kiongozi mmoja wa ngazi za juu wa harakati ya muqawama ya Hizbullah nchini Lebanon amesema kuwa, wapinzani wana nia ya kuing'oa serikali ya Lebanon madarakani. Hayo yamesemwa na Muhammad Raadi mkuu wa mrengo wenye mfungamano na Hizbullah katika bunge la nchi hiyo na kuongeza kuwa, baada ya wapinzani kushindwa kuisambaratisha harakati ya Hizbullah wameazimia kuiangusha serikali ya Najib Miqat sambamba na kuanzisha tuhuma dhidi ya jeshi na vyombo vya usalama vya nchi hiyo. Akiashiria mpango wa kuangusha serikali ya nchi hiyo Raad amesema, hakuna mtu yeyote mwenye haki ya kuvivunjia heshima vyombo vya usalama vya Lebanon hasa kwa kuzingatia kuwa, vikosi vya nchi hiyo vinafanya juhudi kubwa za kulinda usalama na amani wa nchi hiyo.

No comments: