Jumuiya ya Kiuchumi ya Nchi za Magharibi mwa Afrika ECOWAS imetishia kuwawekea vikwazo vipya wafanyamapinduzi wa Mali pamoja na washirika wao. Taarifa ya ECOWAS imesema kwamba, viongozi wapya wa Mali wanafanya njama za kuvuruga amani na uthabiti wa nchi hiyo, ikiwa ni pamoja na kuzuia kuundwa serikali mpya ya kiraia katika nchi hiyo.
Nchi jirani na Mali zimeeleza kutoridhishwa kwao na hatua ya viongozi wa Mapinduzi ya Machi 22 nchini humo ya kuendelea kushikilia hatamu za uongozi wa nchi. Hayo yanajiri katika hali ambayo, hivi karibuni wajumbe wawili kutoka Jumuiya ya Kiuchumi ya Magharibi mwa Afrika ECOWAS waliondoka nchini Mali pasina mafanikio ya kuweza kuyakutanisha pamoja makundi ya kisiasa kushiriki katika serikali ya mseto nchini humo.

No comments:
Post a Comment