Social Icons

twitterfacebookgoogle pluslinkedinrss feedemail

Friday, May 4, 2012

Tunisia yasema kamwe haitakuwa na urafiki na utawala wa Kizayuni

Waziri wa Mambo ya Nje wa Tunisia amesema kuwa, serikali ya Tunisia kamwe haitafanya mahusiano ya kidiplomasia na utawala katili wa Israel. Rafiq Abdul Salam Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Tunisia aliyasema hayo alipokua akijibu ombi la utawala haramu wa Israel lililokuwa linawataka raia wake kufanya safari nchini humo na kusisitiza kuwa, Tunisia kamwe haitafanya mahusiano ya kidiplomasia na utawala huo kwakua unapora haki za Wapalestina sambamba na kukengeuka mikataba ya Kimataifa. Abdul Salam amesema kuwa, nchi yake imevuka hatua nyingi na ndefu hatakama bado yapo baadhi ya matatizo madogo madogo yanayoikabili nchi hiyo hivi sasa. Ameongeza kwa kusema kuwa, hivi sasa Tunisia ipo katika hali nzuri kisiasa na amani na kwamba nchi hiyo inaelekea kwenye mustakbali mwema.

No comments: