Duru ya pili ya uchaguzi wa Majlisi ya Ushauri ya Kiislamu ya Iran (Bunge) imefanyika leo Ijumaa ambapo mamilioni ya wapiga kura wamejitokeza.
Duru hii ya pili imefanyika katika majimbo 33 kote Iran. Wagombea katika majimbo hayo hawakuweza kupata ushindi mutlaki kwenye duru ya kwanza na hivyo wamelazimika kuingia duru hiyo ya pili. Viti vya ubunge vinavyoshindaniwa kwenye duru hii ya pili ni 65. Kwenye duru ya kwanza iliofanyika Machi 2, wabunge 225 kati ya 290 walichaguliwa ambapo asilimia 67 ya wapiga kura milioni 48 walijitokeza.
Katika duru ya kwanza ya uchaguzi mrengo wa wanaotetea misingi ya mapinduzi ya Kiislamu ulipata karibu viti 180 bungeni.
Waziri wa Mambo ya Ndani Iran Mostafa Mohammad Najjar ameelezea matumaini kuwa matokeo ya uchaguzi wa leo yatatangazwa katika kipindi cha masaa 24 yajayo. Ameongeza kuwa uchaguzi umefanyika kote Iran kwa utulivu na bila dosari yoyote
No comments:
Post a Comment