Social Icons

twitterfacebookgoogle pluslinkedinrss feedemail

Friday, May 25, 2012

Sudan na Sudan Kusini zakubaliana kuanza mazungumzo wiki ijayo

Sudan na Sudan Kusini zimekubaliana kuanza mazungumzo wiki ijayo kwa lengo la kumaliza hitilafu zao, baada ya mapigano ya mpakani yaliyotokea wiki kadhaa zilizopita kupelekea mazungumzo ya pande mbili kusimama. El Obeid Marawah msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Sudan amesema mazungumzo hayo yatafanyika tarehe 29 Mei na Sudan Kusini imethibitisha tarehe hiyo. Kiongozi wa timu ya mazungumzo ya Sudan Kusini, Pagan Amum amewaambia waandishi habari kwamba serikali ya Juba ilitaka mazungumzo hayo yafanyike haraka iwezekanavyo na kwamba wamekubaliana kuanza tena mazungumzo hayo Mei 29.
Thabo Mbeki rais wa zamani wa Afrika Kusini ambaye ni mpatanishi wa Umoja wa Afrika katika mgogoro wa nchi hizo mbili wiki hii alikutana na Marais wa nchi hizo katika jitihada za kufufua mazungumzo hayo.

No comments: