Social Icons

twitterfacebookgoogle pluslinkedinrss feedemail

Friday, May 25, 2012

Iran na kundi la 5+1 zakubaliana duru ijayo ya mazungumo ifanyike Moscow

Iran na kundi la 5+1 nchi wanachama wa kudumu wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa na Ujerumani zimekubaliana kuwa duru ijayo ya mazungumo ya pande mbili ifanyike tarehe 18 hadi 19 mwezi June mjini Moscow Russia. Saeed Jalili Katibu wa Baraza Kuu la Usalama wa Taifa la Iran amesema kuwa, anga ya mazungumo na kundi la 5+1 ilikuwa nzuri na kuongeza kuwa mazungumo hayo yalikuwa marefu lakini bado hayajakamilika. Jalili aidha amesema kundi la 5+1 lilikuwa na mapendekezo yake na Iran pia iliwasilisha mapendekezo yake na kwamba matokeo ya mazungumo ya Baghdad ni kuwa kila upande umeweza kuelewa zaidi misimamo ya upande wa pili. Katibu wa Baraza Kuu la Usalama wa Taifa la Iran aidha amesisitiza kwamba urutubishaji urani kwa mujibu wa Mkataba wa N.P.T ni haki ya taifa la Iran isiyoweza kupingika. Kwa upande wake Bi Catherine Ashton Mkuu wa Sera za Nje wa Umoja wa Ulaya ambaye pia ni Mkuu wa timu ya mazungumzo ya kundi la 5+1 amesema kuwa pande hizo mbili zimefikia mtazamo wa pamoja ingawa bado kuna tofauti nyingi.

No comments: