Shirika la Msamaha Duniani Amnesty International limeikosoa serikali ya Angola kwa kuwakandamiza waandamanaji wanaopinga serikali nchini humo. Sambamba na kulaani suala hilo shirika hilo limeitaka serikali ya Angola kuanza kufanya uchunguzi kuhusiana na kushambuliwa waandamanaji na watu waliokuwa na silaha wasiojulikana. Taarifa zinasema kuwa siku ya Jumanne watu wenye silaha wasiojulikana walishambulia nyumba ya mmoja wa viongozi wa maandamanaji wanaopinga serikali na kuwajeruhi watu watatu.
Inafaa kuashiria hapa kuwa, uchaguzi mkuu wa Angola utafanyika Agosti 31 mwaka huu, uchaguzi ambao utakuwa wa pili kufanyika nchini humo tangu kumalizika vita vya ndani vya miaka 27 mwaka 2002.
Inafaa kuashiria hapa kuwa, uchaguzi mkuu wa Angola utafanyika Agosti 31 mwaka huu, uchaguzi ambao utakuwa wa pili kufanyika nchini humo tangu kumalizika vita vya ndani vya miaka 27 mwaka 2002.
No comments:
Post a Comment