Mwendesha mashtaka mkuu katika kesi ya Charles Taylor amependekeza rais huyo wa zamani wa Liberia ahukumiwe kifungo cha miaka 80 gerezani baada ya kupatikana na hatia ya kuhusika na jinai za kivita.
Kwa mujibu wa nyaraka zilizofichuka, Brenda Hollis mwendesha mashtaka mkuu katika Mahakama Maalumu ya Umoja wa Mataifa Kuhusu Sierra Leone huko The Hague, amesema uadilifu utatendeka iwapo Taylor atafungwa miaka 80 gerezani.
Mahakama hiyo maalumu hivi karibuni ilimpata Taylorna hatia ya jinai dhidi ya binadamu. Taylor mwenye umri wa miaka 64 atahukumiwa Mei 30 na iwapo na atahukumiwa kifungo cha jela, anatazamiwa kuhudumu kifungo hicho katika magereza ya Uingereza.

No comments:
Post a Comment