Social Icons

twitterfacebookgoogle pluslinkedinrss feedemail

Friday, May 4, 2012

'Waislamu duniani wakabiliane na wanaoivunjia heshima Qur'ani'

Khatibu wa Sala ya Ijumaa Tehran Ayatullah Sayyed Ahmad Khatami amelaani vikali kitendo cha kasisi wa Marekani cha kuchoma moto nakala za Qur'ani Tukufu na ametoa wito kwa Waislamu wote duniani kukabiliana na kitendo hicho kichafu.

Khatibu wa Sala ya Ijumaa Tehran amesema serikali ya Marekani ni mashirika katika kuvunjiwa heshima Qur'ani na amehoji ni kwa nini Wamarekani ambao hawawezi hata kustahamili mjadala kuhusu maudhui ya 'Holocaust' wanavunjia heshima Kitabu Kitakatifu cha Waislamu zaidi ya bilioni moja na nusu duniani. Ayatullah Khatami pia amekosoa kimya cha Wakristo duniani kufuatia hatua ya kasisi Mkristo Marekani kuivunjia heshima Qur'ani Tukufu. Kuhusu uchaguzi ujao wa rais nchini Misri, Ayatullah Khatami amesema taifa lililostaarabika la Misri halitaruhusu mapinduzi ya wananchi kutekwa. Ameongeza waliohudumu katika utawala wa dikteta Mubarak hawapasi kuchaguliwa na kuongeza kuwa Wamisri watamchagua rais anayepinga ubeberu na Uzayuni. Kuhusu kadhia ya Bahrain, Ayatullah Khatami amesema kuwa, kama ambavyo taifa la Iran linvyounga mkono taifa linalodhulimiwa la Palestina ndivyo litakavyounga mkono taifa linalodhulumiwa la Bahrain.
 

No comments: