Kikao cha hivi karibuni cha Baraza la Ushirikiano la Ghuba ya Uajemi kilifanyika huko Riyadh ambapo suala la muungano baina ya nchi wanachama lilibadilika na kuwa ‘muungano' wa Bahrain na Saudi Arabia.
Duru za habari kieneo na kimataifa zilitathmini pendekezo hilo kuwa sawa na kinga kwa utawala wa Aal Khalifa wa Bahrain ambao unakabiliwa na maandamano na malalamiko makubwa ya wananchi ambapo utawala wa Saudi Arabia unaunga mkono ukandamizaji wa waandamanaji wa Bahrain.
Mfalme Abdullah wa Saudia awashangaza wenzake
Mfalme Abdullah wa Saudi Arabia mwaka mmoja uliopita aliwashangaza viongozi wa nchi za Baraza la Ushirikiano la Ghuba ya Uajemi. Kwa mara ya kwanza ni pale alipotaka Morocco na Jordan ziingizwe katika baraza hilo kama njia ya kukabiliana na wimbi la mwamko wa Kiislamu. Pendekezo lake hilo lilikuwa na lengo la kuunda klabu ya tawala za kifalme katika nchi za Kiarabu na hivyo kuzikinga kutokana na mwamko wa Kiislamu wa wananchi. Mara ya pili Mfalme Abdullah alipowashangaza viongozi wenzake ni pale alipotaka Baraza la Ushirikiano la Ghuba ya Uajemi liondoke kutoka katika kiwango cha ushirikiano hadi 'Umoja na Mshikamano.'
Mfalme Abdullah hakufanikiwa katika pendekezo lake la kutaka Jordan na Morocco zijiunge na Baraza la Ushirikiano la Ghuba ya Uajemi bali hata baadhi ya nchi wanachama zililalamikia vikali pendekezo hilo. Aidha pendekezo la Mfalme Abdullah kuhusu 'umoja' katika Baraza la Ushirikiano la Ghuba ya Uajemi vile vile lililalamikiwa na Oman, Umoja wa Falme za Kiarabu na Qatar. Kuwait imeamua kunyamaza kimya kuhusu pendekezo hilo. Kimya hicho kinamaanisha kuwa Amiri wa Kuwait anapinga mpango huo.
Kama ilivyotarajiwa, aliyeafiki mpango huo ni mtawala wa Bahrain ambaye kwa kipindi cha mwaka mmoja sasa anakabiliwa na wimbi kubwa la maandamano ya wananchi wanaotakademokrasia.
Mwaka mmoja uliopita utawala wa Aal Saud ulituma askari 1000 Bahrain kwa lengo la kuwakandamiza wananchi wanaoupinga utawala dhalimu wa kifalme nchini humo. Watawala wa Saudi Arabia wana wasiwasi mkubwa kuwa mwamko wa watu wa Bahrain utapelekea kuibuka mabadiliko ya kimsingi nchini humo ikiwa ni pamoja na kuanzishwa ufalme wa kikatiba na wimbi hilo kuingia hadi Saudi Arabia.

Mpango wa Saudia kuikalia kwa mabavu Bahrain wapingwa
Makundi ya upinzani na shakhsia wakubwa Bahrain wamepinga mpango wa kuunganishwa Bahrain na Saudi Arabia au kwa ibara sahihi Saudi Arabia kuikalia kwa mabavu Bahrain.
Sheikh Ali Salman Katibu Mkuu wa Chama cha Al Wifaq, ambacho ni chama chenye wafuasi wengi zaidi Bahrain amesma: 'Sisi tunapinga mpango wa shirikisho au fedarali na Saudi Arabia kwani mpango huo unamaanisha Bahrain kuunganishwa na Saudi Arabia. Tunaitaka serikali ya Bahrain isikilize matakwa ya taifa. Utawala wa Kifalme kwa muamala wake mbaya na wananchi unalisukuma taifa katika machafuko. Sera hizi ni potofu na utawala wa kifalme ndio unaopaswa kulaumiwa kwa machafuko nchini.' Ameongeza: ' Bunge na serikali haiwakilishi taifa na uamuzi wowote wanaochukua katika kutekeleza mpango huu ni batili na kinyume cha sheria.'
Kamati ya Habari katika Harakati ya 14 Februari ya Mapinduzi ya Bahrain imetoa taarifa na kusema: 'Enyi watu mabingwa, wapendao uhuru na wanamapambano wa Bahrain, mfahamu kuwa baada ya Saudi Arabia kushindwa kuangusha mapinduzi ya wananchi wa Bahrain hata baada ya kutuma vikosi vyake vya kijeshi sasa inataka kuiunganisha Bahrain na ardhi ya Saudia ili kuwabadilisha Wabahrain kuwa watumwa wa Aal Saudi na hivyo kukanyanga damu ya mashahidi wa Bahrain. Taarifa hiyo imeendelea kusema: 'Baada ya watawala wa Saudi Arabia kulaaniwa na kushinikizwa na nchi mbali mbali na taasisi za kimataifa kutokana na kitendo chao cha kuikalia kwa mabavu Bahrain, sasa wanataka kuiunganisha Bahrain na nchi yao ili kuhadaa fikra za waliowengi duniani na kupunguza mashinikizo dhidi yao kwa lengo la kudhamini usalama wa ndani ya nchi na viti vyao vya kifalme vilivyotikisika. Wana wasi wasi kuwa wimbi la mwamko wa Kiislamu wa wananchi Tunisia, Misri na Yemen utafika nchini humo.'
Baada ya kutangazwa mpango wa kuikalia kwa mabavu Bahrain chini ya kisingizio cha Muungano wa Bahrain na Saudi Arabia, vijana wanamapinduzi wa Bahrain katika hatua isiyo ya kawaida walimiminika katika daraja ya 'Malik Fahad' ambayo ndio njia pekee ya kuunganisha Bahrain na Saudia kwa barabra. Wakiwa hapo waliwasha moto matairi na kufunga daraja hiyo kwa masaa kadhaa. Aidha katika nchi mbali mbali za Kiislamu kulifanyika maandamano makubwa ya kupinga mpango huo hatari wa Saudi Arabia.

No comments:
Post a Comment