Mahakama ya Uturuki imefuta mpango wa serikali wa kubomolewa bustani
iliyo karibu na Medani ya Taksim mjini Istanbul, suala lililozusha
maandamano ya kupinga serikali nchini humo.
Uamuzi wa mahakama hiyo unaonekana kuwa pigo kwa Waziri Mkuu Racep
Tayyip Erdogan aliyekuwa aking'ang'ania mpango huo, na unaonekana kuwa
ushindi kwa wapinzani waliokuwa wakiupinga.
Tangu Mei 31 Istanbul imekuwa ikishuhudia maandamano ya kupinga
serikali huku polisi wakikabiliana na waandamanaji waliokuwa wamepiga
kambi katika Medani ya Taksim kupinga uamuzi wa kubomolewa bustani ya
Gezi. Bustani hiyo imezoeleka kuwa eneo la mijumuiko, mikusanyiko na
maandamano na pia kivutio cha watalii huku ikiwa ni sehemu pekee ya
kijani ya umma iliyobakia kwenye mji wa Istanbul na serikali ilitaka
kuibomoa kujenga maduka.
No comments:
Post a Comment