Social Icons

twitterfacebookgoogle pluslinkedinrss feedemail

Monday, May 14, 2012

Asasi za misaada ya kibinadamu zalaani kubomolewa nyumba za Wapalestina

Uharibifu uliotokana na utawala wa kizayuni wa Israel
Asasi za misaada ya kibinadamu zisizo za kiserikali zimelaani vikali hatua ya kinyama ya utawala wa Kizayuni wa Israel ya kubomoa nyumba za Wapalestina. Mashirika hayo ya kimataifa ya misaada ya kibinadamu yamesikitiswa mno na hatua ya utawala dhalimu wa Israel ya kubomoa nyumba za Wapalestina sambamba na kuharibu miundo mbinu muhimu kama vyanzo vya maji.
Taarifa iliyotolewa na asasi hizo ambazo zinafanya kazi zake chini ya Umoja wa Mataifa imebainisha kwamba, nyumba nyingine zaidi ya mia moja za Wapalestina zimo katika hatari ya kuharibiwa na Israel. Kwa mujibu wa ripoti hiyo, hivi karibuni nyumba 63 za Wapalestina zimebomolewa na utawala wa Kizayuni wa Israel. Hayo yanajiri huku, Israel ikiendelea na ujenzi wa vitongoji vya walowezi wa Kiyahudi katika maeneo ya Wapalestina.

No comments: