Social Icons

twitterfacebookgoogle pluslinkedinrss feedemail

Thursday, May 31, 2012

Uturuki yawa mwenyeji wa mkutano kuhusiana na Somalia

Uturuki imekuwa mwenyeji wa mkutano kuhusiana na Somalia, huku serikali ya Ankara ikiwa moja ya waungaji mkono muhimu wa serikali ya mpito ya nchi hiyo yenye makao yake mjini Mogadishu. Wajumbe kutoka nchi 54 duniani wamekusanyika leo mjini Istanbul ili kutafuta njia itakayowezesha kuwepo mustakbali mzuri kwa ajili ya nchi hiyo ya Kiafrika. Viongozi hao wamesema mwanzoni mwa mkutano huo kuwa, Somalia inahitaji kusaidiwa kukarabatiwa na kufanya jitihada za kurejesha utulivu nchini humo. Bakir Bosdag Naibu Waziri Mkuu wa Uturuki amesema katika mkutano huo kuwa, baada ya kipindi kirefu cha migogoro na kukosekana amani, hivi sasa kuna matumaini ya kupatikana amani na usalama katika siku zijazo nchini Somalia. Waziri Mkuu wa Somalia Abdiweli Mohamedi Ali amesema katika mkutano huo kwamba mustakbali wa Somalia uko mikononi mwa Wasomali wenyewe na kuzitaka nchi wahisani kutoa misaada mbalimbali kwa nchi hiyo.

No comments: